Baada ya kurejea nchini kutoka kwenye majukumu ya timu ya Taifa, mshambuliaji Fiston Mayele amekutana na viongozi wa Yanga kwa ajili ya kujadili hatma yake
Yanga inataka kumbakisha Mayele hivyo wamempa ofa ya kuongeza mkataba wa miaka miwili
Pamoja na wingi wa ofa zilizotua Jangwani kumtaka Mayele, dhamira ya Yanga ni kuona mshambuliaji huyo bora anabaki
Yanga imeweka malengo ya kufanya vizuri msimu ujao hasa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika
Kufikia malengo hayo lazima kuhakikisha inawabakisha wachezaji wake muhimu akiwemo Mayele
Kama makubaliano yatafikiwa huenda siku ya Jumamosi kwenye Mkutano Mkuu, Wanachama wakakutana na habari njema
ADVERTISE HERE