Jumamosi ijayo, March 17 2018 kikosi cha Yanga kitakuwa nchini Botswana kucheza mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Township Rollers.
Kituo cha televisheni cha Azam kupitia chaneli yake ya Azam Sport 2 kitarusha mchezo huo mubashara kutoka nchini Botswana.
Yanga iko nyuma kwa mabao 2-1 kuelekea mchezo huo, inahitaji kushinda angalau mabao 2-0 ili iweze kufuzu hatua ya makundi.
Matokeo ya ushindi mnono iliyopata kwenye michezo miwili ya ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Kagera Sugar na Stand United, yameongeza morali ya wachezaji kuelekea mchezo huo

ADVERTISE HERE