Tutafanya usajili wenye manufaa - Kamwe

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Jun 2023
Tutafanya usajili wenye manufaa - Kamwe

Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema baada ya mafanikio makubwa waliyopata msimu uliomalizika katika michuano yote waliyoshiriki, uongozi umeweka mikakati mikubwa zaidi kuelekea msimu ujao

Baada ya Yanga kuthibitisha kuondoka kwa Kocha Nasreddine Nabi, kumekuwa na tetesi nyingi zinazowahusisha baadhi ya wachezaji kusajiliwa au kuondoka Yanga huku mabingwa hao wa soka Tanzania Bara wakithibitisha kuachana na winga Tuisila Kisinda

Wananchi wana shauku ya kufahamu ni kina nani wamesajiliwa/watasajiliwa katika dirisha la usajili kuelekea msimu ujao ambalo linatarajiwa kufunguliwa Julai 1 2023

Kamwe amesema usajili wa wakati huu hautakuwa kwa ajili ya kuwafurahisha watu, bali utazingatia mahitaji ya timu na malengo waliyojiwekea msimu ujao

"Msimu huu tumeshinda makombe yote ya ndani kama tulivyofanya msimu uliopita. Tumefika fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika, kifuani tumebeba medali nne, haya ni mafanikio makubwa sana"

"Sasa msimu ujao tuna jukumu la kwanza kuhakikisha tunalinda mafanikio haya kwa kushinda mataji yote, pili tunafanya vizuri katika michuano ya ligi ya mabingwa"

"Mara ya mwisho kwa Yanga kucheza hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa ni mwaka 1998, hivyo utaona ni kwa kiasi gani tunahitaji kufanya vizuri katika michuano ya msimu ujao na lengo letu la chini kabisa ni kucheza hatua ya makundi"

"Kila msimu tunafanya usajili lakini usajili wa dirisha hili tutakaofanya utakuwa tofauti zaidi. Utakuwa usajili mzuri wenye manufaa na sio kuwafurahisha watu"

"Nawaambia mashabiki wetu watulie kwani uongozi unajua nini unafanya," alisema Kamwe

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
4h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
7h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
12h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
13h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’