Haikuwa rahisi kwa Yanga kumshawishi Prof Nasreddine Nabi kuendelea kubaki baada ya mafanikio aliyopata katika misimu miwili
Mafanikio makubwa zaidi msimu uliomalizika kucheza fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika yamekuwa chachu kwa Nabi kuzivutia timu nyingi barani Afrika ambazo zina msuli mkubwa wa kifedha kuliko Yanga
Mashabiki na Wanachama wa Yanga hawapaswi kusononeka baada ya Nabi kuondoka, zaidi ni kumshukuru kwa mafanikio aliyoleta Jangwani na kumtakia kila la kheri
Baada ya misimu minne ya kukosa mataji, misimu miwili ya Nabi imekuwa ya kihistoria, kwani ameshinda kila taji la ndani
Jukumu la viongozi wa Yanga ni kuajiri kocha mwingine ambaye ataendeleza pale alipoishia Nabi ili kuleta mafanikio zaidi Jangwani
Ni kawaida makocha bora hupendelea kuondoka pale wamezipa timu mafanikio ili kuacha alama katika klabu zao
Baada ya kushinda mataji sita katika misimu miwili ni wazi presha ingeongezeka kwa Nabi msimu ujao
Jambo jema zaidi ni kuwa Nabi ameondoka katika wakati sahihi msimu ukiwa umemalizika. Yanga ina muda wa kusaka mbadala wake na kuanza majukumu yake ya kuiandaa timu wakati wa pre-season