Leo mkoani Dodoma, klabu ya Yanga imepata heshima ya kukabidhiwa TUZO MAALUM ya kuwa taasisi inayotambulika rasmi na Wizara ya Afya katika uchangiaji wa damu
Waziri wa Afya Mh Ummy Mwalimu alimkabidhi tuzo hiyo Rais wa Yanga Injinia Hersi Said katik madhimisho ya siku ya kuchangia damu Dunia ambayo hufanyika Juni 14 kila Mwaka
Imekuwa ni desturi ya klabu ya Yanga kuchangia damu kupitia kwa wanachama na mashabiki zake kwa lengo la kuokoa maisha ya watanzania wenye mahitaji kama wazazi, wagonjwa waliopata ajali na kadhalika
Ama hakika TUZO hiyo ni heshima kubwa kwa Injinia Hersi ambaye amekuwa mstari wa mbele katika uhamasishaji, pia ni heshima kubwa kwa klabu ya Yanga
ADVERTISE HERE