Mwanamuziki, CEO wa Wasafi Media Nasib Abdul maarufu Diamond Platinumz jana amewapa mashabiki wa Yanga burudani ya aina yake kwenye viwanja vya Jangwani jijini Dar es salaam
Mapema mwaka huu Diamond alitangaza kuihama klabu ya Simba ambayo alikuwa balozi wake na kujiunga na Yanga
Kabla ya kuanza kutumbuiza kwenye shamrashamra za treble, Rais wa Yanga Injinia Hersi Said alimkabidhi Diamond jezi ya Yanga ambayo aliivaa jukwaani
Kwa hakika hakuwaangusha Wananchi, kwani alishusha burudani ya aina yake



Upepo wa Yanga ni kama umewasomba Wasanii wote wenye majina makubwa nchini
Juzi kwenye shamrashamra za ubingwa wa Ligi Kuu tulimshuhudia Rayvanny ambaye pia ametunga wimbo wa kusherehesha mafanikio ya Yanga msimu huu
Huyo Harmonize ni Mwananchi muda mreefu tangu enzi za bakuli, Ali Kiba ndio kabisaaa!
Mario, Dula Makabili, Msagasumu na mastaa wengine wengi wamejipambanua kuwa Wananchi
Kwa hakika kila Mwananchi ni shabiki wa Yanga, kama hataonekana sasa ni suala la muda tu....!