Wakati kikosi cha Yanga kikipaa Tanga kukamilisha msimu kwa mchezo wa fainali kombe la FA dhidi ya Azam Fc, mshambuliaji Fiston Mayele ameelekea DR Congo kwenye majukumu ya timu ya Taifa
Juni 17 na Juni 18 mechi za raundi ya tano kuwania kufuzu fainali za Afcon 2023 zitapigwa ambapo DR Congo itacheza na Gabon Juni 18
Mayele ilikuwa aondoke kabla ya mchezo dhidi ya Tanzania Prisons lakini alibadili safari ili acheze mechi hiyo ili kujihakikishia ufungaji bora wa Ligi Kuu
Aidha kiungo mshambuliaji Stephane Aziz Ki nae ameondoka kwenda kujiunga na timu ya Taifa ya Burkina Faso
Nyota wengine walioitwa timu za Taifa wanatarajiwa kujiunga na timu zao baada ya mchezo dhidi ya Azam fc kesho
Wachezaji wa kigeni waliootwa timu za Taifa ni Djigui Diarra, Khalid Aucho, Stephane Aziz Ki, Kennedy Musonda na Fiston Mayele