Tumerudisha ubabe wetu soka la Tanzania - Hersi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 Jun 2023
Tumerudisha ubabe wetu soka la Tanzania - Hersi

Rais wa klabu ya Yanga Injinia Hersi Said amesema kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu kwa misimu miwili mfululizo ni ishara ya Yanga kurejesha ufalme wake katika soka la Tanzania

Msimu huu Yanga imefikia mafanikio ya juu zaidi kwani pamoja na kutwaa taji la Ligi Kuu, Yanga imecheza fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika pia ikiwa imetwaa Ngao ya Jamii

Yanga itacheza fainali ya kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) dhidi ya Azam mchezo utakaopigwa Jumatatu, Juni 12 uwanja wa Mkwakwani

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii Hersi ameandika;

Leo 9th June 2023 katika jiji la Mbeya, @yangasc wametawazwa kuwa mabingwa wa ligi kuu kwa mara 29.

Furaha na fahari kwa klab hii kubwa nchini kurudisha umiliki wa utawala wake katika soka na mataji nchini.

Moja kati ya kipaumbele cha uongozi wetu ilikuwa ni mataji. Taji la pili msimu huu huku tukileta medali za CAF CC.

Inshallah, Azam federation cup iko mikononi mwetu kwa neema za mola wetu.

Nichukue fursa hii kuwapongeza wachezaji wetu chini ya captain wa mataji @mwamnyeto03
pamoja na benchi la ufundi chini ya coach @nabinasreddine

Niwashukuru sana wadhamini wetu wakuu @tzsportpesa media partner wetu @azamtvtz washirika wetu katika bidhaa @gsmgroupofcompanies wahisani wetu @uniceftz na @afya.drinks.tz

Kwenu wananchi, KESHO TUKUTANE KWENYE PAREDI YA TAIFA!!!!

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
17h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
20h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’