Yanga imekabidhiwa taji la Ligi Kuu ya NBC kwa msimu wa pili mfululizo baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo uliopigwa uwanja wa Sokoine
Wananchi wamekabidhiwa kombe lao katika uwanja wa Sokoine, kama ilivyokuwa msimu uliopita
Ni medali ya tatu msimu huu kuanzia Ngao ya Jamii, Kombe la Shirikisho Afrika na sasa Ligi Kuu
Bado medali moja ya kombe la Shirikisho a Azam (ASFC) siku ya Jumatatu katika mchezo wa fainali dhidi ya Azam Fc
Shamra shamra za ubingwa zimeanza mkoani Mbeya na zitahitimishwa jijini Dar es salaam kesho Jumamosi


ADVERTISE HERE