Wakati mkataba wake ukielekea ukingoni, Bernard Morrison anaendelea kuwashawishi mabosi wa Yanga kumuongeza mkataba kutokana na ubora alioonyesha katika mechi za karibuni
Jana Morrison aliihakikishia Yanga alama moja mkoani Mbeya baada ya kufunga mabao mawili katika mchezo dhidi ya Mbeya City uliomalizika kwa sare ya mabao 3-3 Yanga ikitokea nyuma kwa mabao matatu
Pamoja na kukosekana kikosini kwa muda mrefu kutokana na majeraha, msimu huu Morrison amefunga mabao matano kwenye ligi
Morrison ana takwimu nzuri zaidi za kufunga miongoni mwa mawinga wa Yanga licha ya kucheza dakika chache sana
Yanga inatarajiwa kufanya maboresho katika eneo la washambuliaji wa pembeni ambapo Morrison, Tuisila Kisinda na Jesus Moloko wanatumika
Kisinda atakuwa mchezaji huru baada ya muda wake wa mkopo kufika tamati wakati Moloko na Morrison nao mikataba yao inamalizika
Moloko yuko kwenye majadiliano ya kuongezewa mkataba wakati Morrison na Kisinda bado haijafahamika