Baada ya hafla ya pongezi kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam jana, kikosi cha Yanga kiliondoka Dar kuelekea mkoani Mbeya usiku kwa kutumia ndege maalum waliyopewa na Rais
Yanga iliwasili Mbeya majira ya saa 9 usiku tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbeya City ambao utapigwa leo saa 10 jioni katika uwanja wa Sokoine
Ni wazi Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi leo atalazimika kufanya mabadiliko makubwa ya kikosi chake kutokana na wachezaji wake kuwa na uchovu
Wananchi walicheza fainali ya pili ya kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya USM Alger Juni 03 na leo watashuka tena dimbani mkoani Mbeya
Yanga haikupata muda wa kufanya mazoezi zaidi ya yale ya viungo na misuli