Yanga ndani ya Ikulu ya Tanzania

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 Jun 2023
Yanga ndani ya Ikulu ya Tanzania

Mabingwa wa soka Tanzania Bara Yanga leo wamealikwa Ikulu ya Tanzania na Rais Dk Samia Suluhu Hassan kupata chakula cha jioni na kupongezwa kwa mafanikio waliyopata katika mashindano ya kombe la Shirikisho barani Afrika

Hafla hiyo iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam, imewakutanisha wadau mbalimbali wa soka nchini

Akizungumza katika hafla hiyo, Rais wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan ameipongeza Yanga kwa kufanikiwa kucheza fainali ya kombe la Shirikisho (CAF CC) 

Dk Samia amesema Yanga inastahili pongezi kwa mafanikio hayo ambayo yameitangaza vyema Tanzania

Amewataka Watanzania kuziunga mkono timu za Tanzania zinapocheza Kimataifa kwani sifa ni Tanzania na utani ubaki kwa michuano ya ndani

Katika hatua nyingine, Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amemuomba Rais Samia kuwaongezea eneo la kujenga uwanja Jangwani

Hersi amesema tayari wamekamilisha maandalizi ya awali ikiwa ni pamoja na michoro ya uwanja wanachosubiri ni ruhusa kuanza rasmi ujenzi wa uwanja. Dk Samia amelichukua ombi hilo na kuahidi kulifanyia kazi

Dk Samia pia ameiagiza klabu ya Yanga kutatua mgogoro unaomuhusu mchezaji Feisal Salum 'Fei Toto'

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 30 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 30 2026
1h ago
READ MORE β†’
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
13h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
17h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
22h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
22h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
1d ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’