Mkurugenzi Mtendaji wa Wasafi Media Nasib Abdul 'Diamond' amemzawadia mlinda lango wa Yanga Djigui Diarra Tsh Milioni 10 baada ya kufanya kazi nzuri kwenye mchezo wa pili wa fainali kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya USM Alger
Baada ya kumshuhudia Diarra katika mchezo dhidi ya USM Alger akiokoa mkwaju wa penati, Diamond aliandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii akimsifu na kuwauliza mashabiki wapendekeze zawadi
Diarra leo alikaribishwa Wasafi Media na kukutana na 'suprise' ya kitita cha Tsh Milioni 10
Diarra amemshukuru Diamond kwa zawadi hiyo pia akiwashukuru wote wanaompongeza akiwataka waendelee kuiunga mkono Yanga
ADVERTISE HERE