FT : Yanga 3-1 Stand United

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Mar 2018
FT : Yanga 3-1 Stand United
Yanga leo imeweka rekodi ya kushinda michezo nane mfululizo katika ligi kuu ya Vodacom msimu huu baada ya kuilaza Stand United mabao 3-1 katika mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Yanga iliuanza mchezo huo kwa kasi na ilifanikiwa kuhesabu mabao yake mawili ndani ya dakika 12 yakifungwa na Aly Aly ambaye alitumbukiza wavuni krosi ya Yusuph Mhilu kwenye dakika ya sita na Ibrahim Ajib akifunga bao la pili kwenye dakika ya 12 akimalizia pasi mpenyezo ya Makka Edward.

Katika dakika 30 za mwanzo Yanga ilitawala mchezo na kutengeneza nafasi nyingi lakini kukosekana kwa umakini kuliinyima Yanga mabao zaidi.



Mpaka wakati wa mapumziko Yanga ilikuwa mbele kwa mabao 2-0.

Kipindi cha pili ni Stand United iliyotawala zaidi ikisaka mabao ya kusawazisha huku Yanga ikitumia zaidi mashambulizi ya kushitukiza.

Stand United ilijipatia bao la kwanza kwenye dakika ya 83 kupitia kwa Vitalis Mayanga hata hivyo furaha ya bao hilo haikudumu kwani Obrey Chirwa aliiongezea Yanga bao la tatu dakika moja baadae.

Ushindi huo umeirejesha Yanga katika nafasi ya pili iliyokuwa ikikaliwa na Azam FC kwa muda baada ya kufikisha alama 46.



Yanga sasa imeifikia Simba kw idadi ya alama, timu hizo zikitofautiana kwa mabao pekee.

Simba inaongoza kwa tofauti ya mabao 11 dhidi ya Yanga huku pia ikiwa na mchezo mmoja mkononi.

Aidha mshambuliaji Obrey Chirwa amemaliza ukame wa mabao baada ya kufunga bao lake la 12, akiwa nyuma ya Okwi kwa tofauti ya mabao manne.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’