Kesho Alhamisi saa 5 asubuhi Yanga itaondoka Tanzania kuelekea Algeria kwa ajili ya mchezo wa mkondo wa pili fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya wenyeji wao USM Alger
Mchezo utapigwa Jumamosi, Juni 03 katika uwanja wa July 05 1962, saa 4 usiku kwa saa za Tanzania
July 05 ndio uwanja mkubwa zaidi Algeria ukifunguliwa mwaka 1972, ukiwa na uwezo wa kubeba mashabiki 95,000
Ni uwanja bora wenye viwango vya Kimataifa, hakuna shaka Yanga itakuwa na nafasi ya kudhihirisha ubora wake katika uwanja huo
Mchezo wa kwanza Yanga ilipoteza uwanja wa Benjamin Mkapa kwa kufungwa mabao 2-1 katika mchezo ambao mvua iliathiri kwa kiasi kikubwa mbinu na uchezaji wa Yanga
Yanga inahitaji kupata ushindi wa kuanzia mabao mawili katika dimba la July 05 ili kutwaa taji la CAF CC


