Mapema leo, Mkurugenzi wa Matawi na Wanachama, Haji Mfikirwa, akiongozana na Meneja wa Habari na Mawasiliano, Ally Kamwe walitembelea familia ya marehemu, William Mhebezi (60), aliyefariki dunia akiwa kwenye jitihada za kuingia ndani ya uwanja wa Benjamin Mkapa, kushuhudia mchezo wa Fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF, Yanga va USM Alger, siku ya Jumapili
Wakiwa hapo maeneo ya Kinyamwezi Jijini Dar es Salaam, walitoa salamu za pole kwa niaba ya Uongozi wa Yanga chini ya Rais, Eng Hersi Said kwa familia ya marehemu Mzee Mhebezi
Uongozi wa Yanga unaendelea kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu Familia ya William Mhebezi wapate nguvu na ustahimilivu kwenye kipindi hiki kigumu




Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi. Amen
ADVERTISE HERE