Baada ya kukaa nje kwa zaidi ya miezi minne kutokana na majeruhi, kiungo wa Yanga Thabani Kamusoko amesema anaamini atarejea katika kiwango chake muda sio mrefu.
Kamusoko alicheza kwa dakika 70 katika mchezo wa ligi uliopita dhidi ya Kagera Sugar na Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 3-0.
Katika mchezo huo Kamusoko alicheza vizuri ingawa alishindwa kwenda na kasi ya mchezo, jambo ambalo ni la kawaida kwa mchezaji anayetoka kwenye majeraha ya muda mrefu.
"Kwa sasa najisikia niko vizuri kiafya, sina maumivu tena. Kilichobaki ni kuhakikisha narejea katika kiwango changu," amesema Kamusoko.

ADVERTISE HERE