Nabi, Mayele wapo sana vipi Chivaviro?

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 May 2023
Nabi, Mayele wapo sana vipi Chivaviro?

Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amewataka Wanachama na Mashabiki wa timu hiyo waweke mawazo yao katika mchezo wa fainali kombe la Shirikisho dhidi ya USM Alger ambao utapigwa Jumapili, May 28 katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Kamwe amesema wananchi hawana sababu ya kuyumbishwa na tetesi za usajili zinazosambazwa mitandao nyingine zikiwa na lengo la kuwaondolea 'focus' kuelekea mchezo dhidi ya USM Alger

"Nimeona huko mtandano kuhusu tetesi za Kocha Nabi na mshambuliaji wetu Fiston Mayele kuwa wanawaniwa na timu kubwa"

"Niwahakikishie Wananchi Nabi na Mayele tayari wako kwenye timu kubwa hivyo hawana sababu ya kuondoka. Timu kubwa zinacheza fainali ya michuano ya CAF, Yanga ni miongoni mwa timu kubwa kwani tunacheza fainali ya Shirikisho"

"Pia nimeona tetesi zinazohusiana na mshambuliaji wa Afrika Kusini (Ranga Chivaviro), jambo la uhakika ni kuwa tumesajili mshambuliaji kutoka Afrika Kusini kama alivyosema Rais (Injinia Hersi) katika mahojiano yake na Robert Marawa, tutamfahamu wakati wake utakapofika"

"Kwa sasa tuweke mawazo yetu kwenye mchezo wa fainali ya kihistoria kwa timu yetu. Tuendelee kununua tiketi," alisema Kamwe

Yanga imeingia kambini kujiandaa na mchezo dhidi ya USM Alger ambao Wananchi wamedhamiria kushinda

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’