Nabi afunguka Bacca alivyotuliza safu ya ulinzi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 May 2023
Nabi afunguka Bacca alivyotuliza safu ya ulinzi

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema kuna maboresho makubwa yamefanyika kwenye safu ya ulinzi ambapo kwa sasa wamepunguza makosa mengi waliyokuwa wakiyafanya hapo nyuma

Aidha matumizi ya beki Ibrahim Bacca yameonekana kuinufaisha Yanga hasa kwenye michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika ambapo timu hiyo imeruhusu bao moja tu katika mechi saba ambazo Bacca alicheza

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amekiri kuwa Bacca ameiongezea ubunifu safu yake ya ulinzi na kuondoa baadhi ya makosa huku akikisisitiza kuwa wachezaji wote wamefanya kazi kubwa kwenye kiwanja cha mazoezi kufikia hapa walipofika

"Kuna mabadiriko makubwa safu yetu ya ulinzi, kwa sasa ipo makini na imepunguza makosa madogo madogo yaliyokuwepo na uwepo wa Bacca pia umekuwa imara kutokana na kuwa makini na mipira ya juu changamoto iliyokuwa ikituumiza sasa inaonekana kuondoka"

"Mabeki wetu wanacheza kwa umoja, wanaendeleza kile tunachowaelekeza mazoezini ni furaha kuwa nao kwa pamoja na naamini wanazidi kuimarika na kuelewana siku hadi siku"

Nabi alisema walikuwa wakifungwa sana mabao ya mipira ya kutengwa lakini sasa tatizo hilo analiona linapungua anaamini uwepo wa Bacca na kusogezwa kwa Yanick Bangala namba sita kumeongeza umakini kwenye safu yake ya ulinzi

Nae beki Ibrahim Bacca amesema siri ya mafanikio ya safu ya ulinzi wakati huu ni ushiriano baina ya wachezaji na kufuata maelekezo ya walimu wao

"Ubora wa Yanga ndio umenifanya niwe imara umenipa changamoto ya kujiandaa vizuri kiakili na uwezo wangu binafsi, beki ni eneo linalohitaji umakini wa hali ya juu kwani ukikosea tu unaweza kuigharimu timu. Nilivyokuja Yanga niliwakuta mabeki hawa wakicheza vizuri na kujipa muda wa kupata nafasi na sasa nashukuru ninacheza," 

"Nadhani siri kubwa ni kujituma na kujitoa kwaajili ya timu, ukituangalia wote tunafanya hivyo na kila mmoja kwa nafasi yake anahakikisha hafanyi makosa na hata yakitokea basi anayasawazisha kwa haraka au mwingine anafanya hivyo. Nadhani umoja wetu ndio siri kubwa," alisema Bacca

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
2h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
10h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’