Kwa nini isiwe sisi? Nunua tiketi yako mapema

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 May 2023
Kwa nini isiwe sisi? Nunua tiketi yako mapema

Ni siku tano zimesalia kuelekea mchezo wa kihistoria fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika Yanga ikichuana na USM Alger ya Algeria, Jumapili May 28 katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Kwa nini isiwe sisi? Ni swali ambalo limetumika kama kauli mbiu kuelekea mchezo huo. Inafahamika Mataifa yenye asili ya kiarabu yametawala soka la Afrika kwa miaka mingi

Fainali ya Ligi ya Mabingwa Wydad Casablanca wanachuana na Al Ahly wakati kombe la Shirikisho Yanga wanachuana na USM Alger

Katika fainali hizo, ni Yanga pekee ambayo itawakilisha Mataifa yote yasiyo na asili ya Kiarabu na hapa ndipo Mwananchi unapaswa kuamini kama wao wanaweza basi hata sisi tunaweza

Wakati huu iwe LAZIMA kombe la Shirikisho libaki kwenye ardhi ya Tanzania, hivyo Mwananchi hupaswi kukosa mechi hii ya kihistoria

Ili kutwaa ubingwa Yanga lazima imalize mechi nyumbani kwani inafahamika ni ngumu sana kupata matokeo ya ushindi ugenini hasa kwa nchi hizi za kiarabu inapofika hatua kama hizi za fainali

Pamoja na kuwa msimu huu Yanga imekuwa na matokeo mazuri katika mechi za ugenini, lakini ni lazima kujihakikishia ushindi mnono nyumbani ili mechi ya ugenini iwe ya kulinda ushindi na kukamilisha ratiba

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
12h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
16h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
17h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
17h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
22h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’