Baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Marumo Gallants na kukata tiketi ya fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika, kikosi cha Yanga kimeondoka Mji wa Rustenburg mapema leo kuelekea Johanesburg, Afrika Kusini
Yanga itaondoka Afrika Kusini leo kurejea Tanzania ambako Jumapili, May 21 inakabiliwa na mchezo wa nusu fainali kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) dhidi ya Singida BS ambao utapigwa uwanja wa LITI mkoani Singida
Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amewataka Wanachama na Mashabiki wa timu hiyo kuendelea kuiunga mkono timu yao ili kuhakikisha wanatimiza malengo
Kamwe amesema huu sio wakati wa shamrashamra, wanahitaji kushinda mchezo dhidi ya Singida BS na kutinga fainali ya ASFC
"Nawaambia Wanachama na Mashabiki wetu, waendelee kutuunga mkono, muda wa shamrashamra bado, wasije uwanja wa ndege kutupokea kwani bado hatujamaliza kazi, tunakabiliwa na mechi mbili muhimu ambazo ni nusu fainali FA na fainali ya Shirikisho Afrika," alisema Kamwe






