Majira ya saa 1 usiku Yanga itashuka uwanja wa Royal Bafokeng kumenyana na Marumo Gallants katika mchezo wa mkondo wa pili nusu fainali kombe la Shirikisho barani Afrika
Ni mchezo muhimu kwa Yanga kushinda au kupata sare ili kujihakikishia tiketi ya kutinga fainali ya michuano hiyo
Marumo walitangaza mashabiki wataingia bure katika mchezo huo utakaopigwa kuanzia saa 12 jioni kwa saa za Afrika Kusini ambapo kwa Tanzania itakuwa saa 1 usiku
Jambo la uhakika ni kuwa Yanga haitaingia kinyonge kwani itakuwa na sapoti kubwa ya mashabiki
Watanzania wengi wanaoishi Afrika Kusini wameweka Utanzania wao mbele ambapo mamia wamesafiri Rustenburg kwa ajili ya kuipa sapoti Yanga
Yanga pia iliondoka jijini Dar es salaam na msafara wa takribani watu 100 ambao wameungana na msafara mwingine wa mashabiki waliosafiri kwa basi ambao walitua Afrika Kusini mapema asubuhi
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iligharamikia mashabiki 55 ambao wameongozwa na Naibu Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo Mh Hamis Mwinjuma ambaye yuko Afrika Kusini toka jana
Mfadhili/Mdhamini wa Yanga Ghalib Said Mohammed 'GSM' nae atakuwepo uwanjani akiwa sambamba na viongozi wa Yanga na wadau wengine wote waiosafiri kwa lengo la kuipa sapoti Yanga katika mchezo huo
Itoshe kusema Wananchi wako tayari kuuwasho moto katika uwanja wa Royal Bafokeng kuhakikisha Yanga inapata matokeo yatakayo wavusha fainali