Yanga Princess inakamilisha ligi kuu ya Wanawake leo ugenini kwa mchezo dhidi ya Amaan Queens katika uwanja wa Ilulu, Lindi
Haukuwa msimu mzuri kwa Yanga Princess ambayo imemaliza nafasi ya nne katika msimamo wa ligi nyuma ya JKT Queens, Simba Queens na Foutain Gate Princess
Makamu wa Rais wa Yanga Arafat Haji amesema watafanya maboresho ya kikosi kwa mara nyingine kwa kusajili wachezaji bora zaidi katika maeneo yaliyokuwa na changamoto
Kwa kiasi kikubwa Yanga Princess imekuwa na changamoto katika safu yake ya ushambuliaji kwani timu imekuwa ikitengeneza nafasi nyingi lakini imefunga mabao machache
JKT Queens ina nafasi ya kutwaa ubingwa ikiwa inaongoza ligi na alama 43 huku ikikamilisha mechi ya mwisho dhidi ya Mkwawa Queens inayoburuza mkia ikiwa tayari imeshuka daraja