Taarifa iliyoripotiwa na kupewa uzito mkubwa Afrika Kusini leo ni wachezaji wa Marumo Gallants kugoma kufanya mazoezi kwa kile kilichoelezwa madai ya posho
Mtandao wa FARPost uliripoti taarifa hiyo mapema leo na kunukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari Afrika Kusini na hapa Tanzania
Wanasema vitani kila aina ya silaha inaweza kutumika, ni wazi hii ni mbinu tu ambayo Gallants wanaitumia ili kuwapumbaza Yanga waamini timu hiyo ina mgogoro
Hata hivyo wamefeli kwani Yanga inaendelea na mipango yake kuelekea mchezo utakaopigwa kesho Jumatano katika uwanja wa Royal Bafokeng
Leo Yanga itakamilisha mazoezi ya mwisho saa 12 jioni kwa saa za Afrika Kusini ikiwa ni saa 1 usiku kwa saa za Tanzania
ADVERTISE HERE