FT : Yanga 3-0 Kagera Sugar

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 Mar 2018
FT : Yanga 3-0 Kagera Sugar
Mabingwa wa ligi kuu ya Vodacom Yanga wamerejea rasmi kwenye mbio za kutetea ubingwa wao kwa msimu wa nne baada ya kuilaza Kagera Sugar mabao 3-0 katika mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa.

Yanga iliuanza mchezo huo taratibu na kuwapa Kagera Sugar nafasi ya kutawala mchezo kwa muda mwingi hata hivyo ilifanikiwa zaidi kupitia mashambulizi ya kushitukiza.

Mabao yote ya Yanga yalipatikana kwenye kipindi cha pili yakifungwa na Ibrahim Ajib kwa mkwaju wa penati kwenye dakika ya 55 baada ya mlinzi wa Kagera Sugar kuunawa mpira aliokuwa ameupigwa mwenyewe.



Aidha kuingia kwa Yusuph Mhilu aliyechukua nafasi ya Thabani Kamusoko kwenye dakika ya 70 kuliiongezea Yanga kasi ya mashambulizi.

Yanga iliandika bao la pili kwenye dakika ya 76 baada ya krosi ya Ibrahim Ajib kufika mguuni kwa Obrey Chirwa ambaye aliwatengea Emanuel Martin na Yusuph Mhilu ambao ni kama waliutumbukiza mpira kimiani kwa pamoja.

Yusuph Mhilu ndiye aliyepeleka majanga kwa Kagera Sugar ambapo krosi yake kwenye dakika ya 88 ilitua miguuni kwa Shemvuni aliyejifunga.

Ushindi wa mabao 3-0 leo umeiwezesha Yanga kufikisha alama 43 sasa ikitofautiana na Simba kwa tofauti ya alama tatu, Simba ikiwa na alama 46.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
6h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
7h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
17h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
20h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1d ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’