Mlinzi wa Yanga Ibrahim Hamad Bacca amewashukuru mashabiki wa Yanga wanaendelea kumtia hamasa ili aendelee kufanya vizuri
Bacca amekuwa katika kiwango bora tangu Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amuamini na kumtumia katika kikosi cha kwanza
Bacca amekuwa na takwimu za aina yake katika kikosi cha Yanga akicheza mechi sita kwenye kombe la Shirikisho barani Afrika huku mechi zote Yanga ikifanikiwa kuondoka na cleansheet
"Mpira ni mchezo wa wazi, mashabiki wanaona kile ninachofanya uwanjani hivyo nawashukuru kwa maoni yao na kunitia moyo ili niendelee kufanya vizuri zaidi. Lakini pia nawashukuru hata wale wanaozungumzia mapungufu yangu kwani wananisaidia kuimarika," alisema Bacca
Bacca ambaye uongozi wa Yanga uko katika hatua za mwisho kumsainisha mkataba wa miaka mitatu, amesema msimu huu umekuwa bora sana kwao katika michuano ya Kimataifa lengo lao likiwa kutinga fainali
Beki huyo kisiki alibainisha mbinu walizotumia jana katika mchezo ya Marumo Gallants wakifanikiwa kuwadhibiti nyota wa timu hiyo ambao kabla ya kukutana na Yanga walifunga bao katika kila mchezo
"Marumo ni timu nzuri, ina wachezaji wenye ubunifu ambao wanacheza soka la Ki Afrika Kusini. Tulibaini wachezaji wao wenye madhara na kuwaacha wacheze mpira katika maeneo ambayo hawawezi kutudhuru. Tumepata ushindi nyumbani, naamini kama tutaongeza bidii katika mchezo wa pili hawawezi kutusumbau huko kwao"
"Lengo letu ni kupata matokeo mazuri Afrika kusini na kutinga fainali. Hili ni hitaji la kila mchezaji"