Yanga leo inashuka uwanjani wa Taifa/Uhuru kuumana na Kagera Sugar kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom mzunguuko wa 21.
Mchezo huo unaweza kuhamishiwa kwenye uwanja wa Uhuru kama mazingira ya uwanja wa Taifa hayakuwa ya kuridhisha.
Juzi uwanja huo ulijaa maji kutokana na mvua kubwa iliyonyesha jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Yanga Hafidh Saleh amesema kuwa kiungo Thabani Kamusoko anaweza kutumika leo (japo kwa dakika chache).
Amesema Kamusoko hakupangwa kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Township Rollers Jumanne iliyopita kwa kuwa hakuwa fiti kwa asilimia miamoja.
"Kesho (leo) Kamusoko anaweza akacheza lakini si kwa dakika zote 90, ametoka kuwa majeruhi hivyo atapewa muda mdogo ili kuendelea kuimarika," amesema Saleh.
Endapo Yanga itafanikiwa kuibuka na ushindi kwenye mchezo wa leo, itakuwa imepunguza pengo la pointi baina yao na vinara Simba na kufikia pointi tatu na kuendelea kuchochea ushindani kwenye kuwania ubingwa msimu huu.
Kiungo Raphael Daud na Geofrey Mwashiuya wataukosa mchezo huo kutokana na kutumikia adhabu ya kadi tatu za njano.

ADVERTISE HERE