Hatuna taarifa ujio wa Marumo Gallants - Kamwe

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 May 2023
Hatuna taarifa ujio wa Marumo Gallants - Kamwe

Klabu ya Marumo Gallants kutoka Afrika Kusini ambayo itachuana na Yanga kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika bado haijawasili nchini na haijafanya mawasiliano na klabu ya Yanga

Kwa mujibu wa kanuni za CAF, Yanga ikiwa mwenyeji wa mchezo huo ina jukumu la kuwapokea wageni wao na kuhakikisha wanapata huduma zote muhimu ikiwa ni pamoja na kuwapa usafari kutoka uwanja wa ndege mpaka hoteli watakayofikia

Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema klabu imefanya jitihada muhimu za kuwasiliana na Marumo lakini hawajajibu wala kutoa taarifa juu ya ujio wao

Hata hivyo Kamwe amesema wanazo taarifa ambazo sio rasmi kuwa klabu hiyo huenda ikawasili nchini mapema Jumanne ikiwa ni siku moja kabla ya mchezo dhidi ya Yanga

"Ni kweli hatuna taarifa za ujio wa Marumo Gallants. Tuliwaandikia barua kuwauliza wanakuja lini Tanzania hili ni jambo la kikanuni kabisa lakini hawakujibu hivyo mpaka hivi sasa hatujui wanakuja lini. Ila za ndani kabisa baada ya kufanya research yetu tumebaini wanakuja kesho asubuhi," alisema Kamwe

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
2h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
7h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
8h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
18h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1d ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’