Azam Fc imetangulia fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) baada ya kuichapa Simba mabao 2-1 katika mchezo wa nusu fainali uliopigwa uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara
Azam Fc walikuwa bora katika mchezo huo, ushindi ni matokeo ambayo walistahili
Ni shangwe kwa mashabiki wa Azam Fc baada ya kuishuhudia timu yao ikizima tambo za Simba na kuwaacha wakimaliza msimu pasipo taji lolote
Azam Fc itachuana na mshindi wa mchezo wa pili wa nusu fainali kati ya Singida BS dhidi ya Yanga ambao utapigwa May 21 uwanja wa LITI
Kabla ya kuikabili Singida BS, Wananchi wanajukumu la kuisaka fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika kwa mchezo dhidi ya Malumo Gallants
ADVERTISE HERE