Kwa sasa mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele ni miongoni mwa washambulizaji bora barani Afrika
Kasi yake katika kupachika mabao imemfanya kuwa mchezaji anayezungumzwa zaidi huku klabu nyingi zikionekana kuvutiwa nae
Ndivyo ilivyo, kila timu inapenda kuwa na mchezaji bora, ofa nyingi zinamiminika Jangwani kumtaka Mayele, lakini hapatikani kirahisi
Hivi karibuni zilivumaa tetesi mitandaoni kuwa klabu ya Vipers Fc kutoka Uganda imewasilisha ofa Jangwani kumtaka Mayele kwa Tsh Milioni 200
Imethibitika zilikuwa 'porojo' za mitandaoni tu kwani Vipers Fc hawana 'msuli' wa kuweza kumsajili Mayele
Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa Yanga zimedokeza kuwa thamani ya Mayele sio chini Tsh Bilioni 2
Hivyo kwa klabu yoyote itakayomuhitaji Mayele itahitaji kujipanga