Msuva tayari ana mabao manne ligi ya mabingwa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Mar 2018
Msuva tayari ana mabao manne ligi ya mabingwa
Jana winga Simon Msuva aliifungia Difaa Al Jadida bao pekee kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Difaa Al Jadida ilishinda kwa bao 1-0

Katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Ben Ahmed El Abdi mjini El Jadida, Mazghan, Msuva mchezaji wa zamani wa Yanga ya Dar es Salaam alifunga bao hilo dakika ya nane, ambalo linakuwa la nne kwake katika michuano hiyo msimu huu, kufuatia kufunga hat-trick katika mchezo wa kwanza dhidi ya Benfica Bissau ya Guinea Bissau.

Difaa Al Jadida sasa watatakiwa kwenda kuulinda ushindi wao huo mwembamba kwenye mchezo wa marudiano mjini Kinshasa siku 10 zijazo.

Tangu atue klabu hiyo mwanzoni mwa msimu huu Msuva amekuwa na mwenendo mzuri wa upachikaji mabao sasa akiwa amefunga mabao 12 katika michuano yote.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
7h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
15h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
18h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
22h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’