Baada ya jana kushindwa kutua mkoani Dodoma kutokana na changamoto ya taa katika uwanja wa ndege wa Dodoma na hivyo kulazimika kurejea jijini Dar es salaam, masafara wa Yanga umeondoka Dar mapema leo kuelekea Dodoma
Baada ya kutua Dodoma, Yanga itaunganisha kwa basi kuelekea Singida wanakokabiliwa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Singida BS utakaopigwa uwanja wa Liti, Alhamisi May 04
Ni matumaini TFF itasikiliza maombi ya Yanga na kusogeza mbele mchezo wa nusu fainali kombe la FA unaopaswa kupigwa May 07 ili Yanga irejee Dar baada ya mchezo dhidi ya Singida BS kujiandaa na mchezo wa CAF Shirikisho dhidi ya Malumo Galants utakaopigwa May 10
ADVERTISE HERE