Fiston Mayele ameendelea kuitikisa Afrika kutokana na umahiri wake katika kuzifumania nyavu katika michuano ya kombe la Shirikisho barani
Bao la kwanza alilofunga kwenye mchezo dhidi ya Rivers United uliopigwa Nigeria limempa tuzo ya pili ya goli bora la wiki
Mayele pia alishinda tuzo ya goli bora katika mchezo dhidi ya US Monastir uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa, likiwa ni goli la pili la Yanga katika ushindi wa mabao 2-0
Ikumbukwe Mayele yuko kileleni katika vita ya kuwania ufungaji bora katika michuano ya Shirikisho akiwa sambamba na Chivaviro wa Malumo Galants wote wakiwa wamefunga mabao matano
A counterattack straight out of the textbooks!@yangasc1935βs Fiston Mayeleβs finish earns the #TotalEnergiesCAFCC #GoalOfTheWeek! pic.twitter.com/fT8YafBYSD
— TotalEnergies CAFCL - TotalEnergies CAFCC (@CAFCLCC) April 26, 2023