Kikosi cha Yanga kimerejea salama Dar es salaam wakitokea Nigeria ambako walifanikiwa kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Rivers United katika mchezo wa mkondo wa kwanza robo fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika
Baada ya kuwasili, Wananchi wameelekea moja kwa moja kambini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa marudiano ambao utapigwa Jumapili, April 30 2023
Yanga imepania kutinga nusu fainali ya michuano hiyo ikihitaji ushindi au matokeo ya sare katika mchezo wa mkondo wa pili utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
ADVERTISE HERE