Pamoja na kusafiri na kikosi cha Yanga nchini Nigeria, winga Bernard Morrison hakuwa sehemu ya kikosi kilichopata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Rivers United katika mchezo wa mkondo wa kwanza robo fainali kombe la Shirikisho la CAF
Yanga imefafanua kwa nini Morrison hakucheza mchezo huo licha ya kuwa sehemu ya wachezaji waliofanya maandalizi ya mwisho siku ya Jumamosi
Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze amesema Morrison alipata changamoto ya misuli kwenye mazoezi ya mwisho hivyo waliona sio vyema kumtumia ili aweze kupona majeraha hayo madogo
"Morrison alipata shida kidogo ya msuli kwenye mazoezi ya mwisho, kama benchi la ufundi tukaona sio sawa kumlazimisha acheze kwani anaweza kuumia zaidi," alisema Kaze
Tangu arejee kikosini baada ya kupona majeraha yaliyomuweka nje kwa miezi minne, Morrison bado hajawa fit kwa asilimia 100 kuweza kuitumikia Yanga
Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi alimpa dakika 15-20 kwenye baadhi ya mechi zilizopita