Leo Yanga itashuka uwanja wa Godswill Akpabio International ikiwa na lengo moja tu, kusaka matokeo ya ushindi ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho la CAF
Kama ushindi utapatikana, ina maana Yanga itakuwa imerahisisha kazi kuelekea mchezo wa marudiano utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa wiki ijayo
Hautakuwa mchezo mwepesi, Rivers United ni timu ngumu inapocheza katika uwanja wake wa nyumbani pamoja kuwa dimba la Godswill Akpabio wanalitumia baada CAF kuwagomea kutumia uwanja wao wa Adokiye Amiesimaka ulio katika mji wa Port Harcourt
Yanga imekuwa na maandalizi mazuri Nigeria ikikwepa mbinu chafu za wapinzani wao, Wanigeria wanapaswa kujua kazi wanayo leo!
Pamoja na kusaka ushindi, kwa Yanga hii ni kama mechi ya kisasi, Rivers United wanapaswa kupigwa hapo hapo kwao kama walivyofanya wao mwaka 2021 kwa kupata ushindi katika uwanja wa Benjamin Mkapa katika mchezo wa hatua ya awali ligi ya mabingwa
Wachezaji wa Yanga wako tayari na wameahidi furaha kwa Wananchi, muhimu ni kuongeza dua ili ushindi upatikane huko Nigeria leo
