Tumebaini kilichotukwamisha - Nsajigwa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 Mar 2018
Tumebaini kilichotukwamisha - Nsajigwa
Kocha Msaidizi wa Yanga Shedrack Nsajigwa amesema timu yake ilichapwa mabao 2-1 na Township Rollers jana kwa kuwa haikucheza vizuri.

Nsajigwa amewasifu Township Rollers kwa kusema walicheza kitimu zaidi na amewapongeza kwa ushindi huo walioupata ugenini.

Nsajigwa amesema kilichopelekea Yanga kupoteza mchezo huo ni kitendo cha kuwaruhusu wapinzani wao wamiliki mpira kwa muda mrefu hasa kwenye kipindi cha pili.

Lakini amesisitiza kuwa wameyabaini makosa yao na sasa wanajipanga kwa ajili ya mchezo wa marudiano unaopigwa March 17.

"Tumeshajua wapi ambapo tumekosea baada ya mchezo huu, tuliwaacha sana wenzetu wacheze, kikubwa tunajipanga kwa ajili ya mechi ijayo," amesema Nsajigwa.

"Wenzetu wamecheza kitimu zaidi wakati sisi tumefanya makosa mengi sana. Tutahakikisha makosa haya hayajirudii kwenye mchezo wa marudiano."

Naye kocha wa Township Nikola Cavazovic amesema amekuwa akiifuatilia Yanga kwa wiki tatu na kubaini aina yao ya mchezo.

Amewasifu wachezaji wake kwa kuibuka na ushindi huo muhimu wa ugenini lakini amesema bado anaiheshimu Yanga na anadhani bado watakuwa na kazi ya kufanya kwenye mchezo wa marudiano nyumbani, March 17.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
6h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
10h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
15h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
15h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’