Kikosi cha Yanga leo kinaondoka jijini Lagos kuelekea Mji wa Uyo kukamilisha maandalizi kuelekea mchezo wa mkondo wa kwanza robo fainali kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Rivers United
Mtanange huo utapigwa siku ya Jumapili, April 23 majira ya saa 10 jioni kwa saa za Tanzania
Meneja wa Yanga Walter Harrison amesema watakuwa na siku mbili za kufanya mazoezi katika Mji wa Uyo kuanzia leo na Jumamosi watakamilisha maandalizi yao katika uwanja wa Godswill Akpabio International ambao utatumika siku ya Jumapili
Yanga inahitaji kushinda mchezo huo hata matokeo ya sare ugenini kabla ya mchezo wa marudiano ambao utapigwa wiki ijayo, April 30 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
ADVERTISE HERE