Wasichokijua wale wanaoibeza Yanga

Muungwana wa Yanga By Muungwana wa Yanga
β€’
7 Mar 2018
Wasichokijua wale wanaoibeza Yanga
Michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika ndio michuano mikubwa kabisa kwa ngazi ya vilabu kwa kuwa inashirikisha vilabu mabingwa wa nchi zao.

Kipigo cha mabao 2-1 walichofungwa Yanga na Township Rollers nyumbani ni matokeo ambayo yamemuuma kila Mwana Yanga lakini wakati mwingine inabidi kukubali kwa kuwa ndio hali halisi.

Yanga sasa ni kama ina kikosi kipya kilichosheni vijana wengi ambao wengine ndio kwanza wanapata uzoefu wa michuano ya Kimataifa.

Wachezaji wengine walikuwepo miaka iliyopita lakini wakati huo hawakuwa wakiaminiwa kama ilivyo sasa.

Yanga imepita katika misukosuko mingi sana msimu huu lakini vijana wamekuwa wakipambana kwa hali na mali kuhakikisha hawaangushi mashabiki.

Huu ni mchezo wa pili kwa Yanga kupoteza msimu huu watatu ukijumlisha na ule wa nusu fainali kombe la Mapinduzi.

Kikosi ni hikihiki. Kupoteza mchezo wa leo hakuwaondolei wachezaji ushujaa ambao wamekuwa wakionyesha tangu mwanzoni mwa msimu.

Bado Yanga itacheza na Township Rollers katika mchezo wa marudiano siku 10 zijazo. Ni muhimu kuweka akiba ya maneno.

Mchezo wa pili hautakuwa na presha kwa Yanga kama ulivyokuwa wa leo.

Leo wachezaji walikuwa na presha kwa kuwa walikuwa wakicheza mbele ya mashabiki wao na hawakupenda kupoteza mchezo huo.

Mchezo wa marudiano Yanga haitakuwa na hofu ya kufungwa kwa sababu tayari wako nyuma.

Watacheza mchezo wa kushambulia zaidi wakati hali inaweza kuwa tofauti kwa wenyeji wao Township Rollers ambao wanaweza kudhani wameshamaliza kazi ugenini.

Hata ikitokea Yanga ikaondoshwa katika hatua hii na Township Rollers, bado itaendelea kubaki kwenye michuano ya Kimataifa kwani itashushwa kwenye michuano ya kombe la shirikisho.

Michuano hii ambayo klabu ya Simba inashiriki.

Ikiwa hivyo Yanga itapangiwa kucheza na moja ya timu zitakazofuzu raundi hii ya kwanza ambapo kama ikishinda itatinga hatua ya makundi.

Hivyo kufungwa na Township Rollers sio mwisho wa ushiriki wa michuano ya Kimataifa msimu huu.

Muhimu ni kwamba bado Yanga ina dakika nyingine 90 za kubadili matokeo na kusonga mbele. Haijalishi itakuwa ugenini.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
6h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
21h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’