Hesabu za Yanga ziko salama kuelekea ubingwa wa ligi kuu kwa msimu wa pili mfululizo
Mechi 26, alama 68 tano juu ya timu inayofuata katika nafasi ya pili ambayo ni Simba
Yanga imekuwa na msimu bora kuliko timu zote mpaka sasa, takwimu zinazungumza
Yanga ndio timu iliyoshinda mechi nyingi nyumbani na ugenini kuliko timu yoyote katika ligi msimu huu
Ubingwa uko mikononi mwa Wananchi, jukumu la wachezaji wa Yanga ni kuhakikisha wanaubeba
Hao wengine wanazungumzia ubingwa lakini wanafahamu hawawezi kuupata bila makosa ya Yanga
Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi ameahidi hawatafanya makosa katika mechi nne zilizobaki na kuwa watacheza kila mechi kama fainali


ADVERTISE HERE