Mwishoni mwa wiki hii Jumapili, April 23 2023, Yanga itakuwa nchini Nigeria kwa ajili ya mchezo wa mkondo wa kwanza robo fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Rivers United
Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) limethibitisha teknolojia ya usaidizi wa waamuzi kwa njia ya video (VAR) itaanza kutumika kuanzia mechi za robo fainali kwenye ligi ya mabingwa na kombe la Shirikisho
Wengi wanakumbuka mechi ya mwisho Yanga kuchuana na Rivers United huko Nigeria mwaka 2021 kwenye ligi ya mabingwa hatua za awali, kulikuwa na matukio mengi ya nje ya uwanja kabla na hata wakati wa mchezo wenyewe
Lakini kwa uwepo wa VAR hii ni habari njema kwani kutakuwa na uzingatia wa sheria 17 za soka hasa kwa yale matukio tata
Wachezaji wanapaswa kuandaliwa wajiepushe na matukio yoyote yasiyofaa kwani kutakuwa na camera zinazochukua matukio hayo