Twendeni Nigeria kwa tahadhari - Manara

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Apr 2023
Twendeni Nigeria kwa tahadhari - Manara

Msemaji wa zamani wa klabu ya Yanga Haji Manara amesema timu inapaswa kwenda Nigeria ikichukua tahadhari zote kuhakikisha wanapata matokeo mazuri ugenini

Manara amesema viongozi, benchi la ufundi, wachezaji, mashabiki na Wanachama hawapaswi kuwekwa vichwani mwao matokeo ya mchezo dhidi ya Simba, kwani umeshapita

Amesema Yanga inapaswa kujipanga vyema kuhakikisha wanaweza kupata ushindi dhidi ya Rivers United na kutinga nusu fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika

"Tuna mechi muhimu sana Nigeria, tunapaswa tuweke nguvu zetu huku ili kuhakikisha tunakwenda kufanya vizuri ugenini na kuja kumaliza kazi nyumbani"

"Hatuna sababu ya kuendelea kufikiria matokeo ya mchezo uliopita dhidi ya Simba, zaidi tutumie kama funzo kuelekea mchezo unaofuata, hatupaswi kuwadharau wapinzani wetu"

"Huu ni wakati wa kazi sasa, tuache maneno mengi kabla ya mechi, twende tukaipiganie nembo ya Yanga na kuweka historia kubwa katika soka la Tanzania," alisema Manara

Yanga inakabiliwa na mchezo wa mkondo wa kwanza robo fainali kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Rivers United ambao utapigwa Jumapili, April 23 huko Nigeria

Yanga itakwenda Nigeria ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza dhidi ya Rivers United mwaka 2021 katika michuano ya ligi ya mabingwa

Mechi ya mkondo wa pili itakamilishwa jijini Dar es salaam katika uwanja wa Benjamin Mkapa, April 30

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
7h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
11h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
16h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
16h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
20h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’