Kipigo cha mabao 2-0 dhidi ya Simba sio matokeo ambayo Wananchi waliyatarajia leo, lakini ndio mpira ulivyo
Yanga imekuwa bora katika mechi nyingi, inapotokea ikapoteza mchezo katika mazingira kama ya leo, jambo pekee ambalo Mwananchi unapaswa kufanya ni kukubali matokeo na kusonga mbele
Bado Yanga iko kileleni mwa msimamo wa ligi kwa tofauti ya alama tano, focus inabaki kwenye kutetea ubingwa, kuna mechi nne za kukamilisha hilo
Hakuna muda wa kulaumiana hasa ikizingatiwa timu inapaswa kusafiri Nigeria kwa ajili ya mchezo wa mkondo wa kwanza robo fainali kombe la Shirikisho dhidi ya Rivers United
Matokeo ya leo yatamsaidia kocha Nasredine Nabi na benchi lake la ufundi kubaini ni maboresho yapi anapaswa kufanya ili kuhakikisha ushindi unapatikana katika mchezo unaofuata
Itoshe kusema vijana walikuwa na siku mbaya ofisini, Yanga bado iko imara!