Nani anaanza, nani anasubiri leo?

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Apr 2023
Nani anaanza, nani anasubiri leo?

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi leo anaongoza timu yake katika mechi ya tisa ya derby dhidi ya Simba

Mtanange huo utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa saa 11 jioni, una umuhimu wa kipekee kwa Yanga kushinda ili kujihakikishia ubingwa wa ligi kuu ya NBC mapema

Habari njema kwa Nabi na benchi la ufundi ni kuwa nyota wake wote wako tayari kutumika katika mchezo huo

Watakaokosekana ni mlinda lango Aboutwalib Mshery (majeruhi) na beki Mamadou Doumbia ambaye amesafiri nchini Mali kushiriki msiba wa Baba yake Mzazi

Nabi amekuwa hatabiriki kutokana na mabadiliko ya kikosi chake kutoka mchezo mmoja na mwingine

Hii ndio faida ya kuwa na kikosi kipana kulinganisha na mpinzani wake Robertinho Oliveira ambaye kikosi chake kinafahamika hata kabla ya kutangazwa

Ni wazi leo Nabi ataanza na kikosi kilicho tayari kucheza soka la kasi kutumia madhaifu ya safu ya ulinzi ya Simba

Lakini pia Yanga leo inahitaji kuwa imara na makini katika eneo la kiungo ili kuhakikisha hawatoi mwanya kwa wapishi wa Simba ambao ni Saido Ntibazonkiza na Clatous Chama

Huenda Nabi leo akatumia kikosi alichokitumia katika mchezo dhidi ya US Monastir kwa kuwaanzisha kennedy Musonda, Fiston Mayele na Jesus Moloko katika safu ya ushambuliaji

Huku eneo la kiungo akiwaweka Yannick Bangala, Khalid Aucho na Salum Abubakar 'Sure Boy' wakati Djigui Diarra, Juma Shaban, Joyce Lomalisa, Ibrahim Bacca/Dickson Job na Bakari Mwamnyeto wakinza safu ya ulinzi

Stephane Aziz Ki, Mudathir Yahya na Bernard Morrison nao wanaweza kuwa na nafasi katika mchezo huo ambao Yanga inasaka ushindi ili kufunga hesabu za ubingwa wa ligi kuu mapema

Yanga leo itashuka dimbani ikiwa katika uzi wake wa bahati, NYEUSI

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’