FT : Yanga 1-2 Township Rollers

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 Mar 2018
FT : Yanga 1-2 Township Rollers
Yanga imejiweka kwenye mazingira magumu kufuzu hatua ya makundi michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Township Rollers katika mchezo wa kwanza uliopigwa kwenye dimba la Taifa.

Dalili hazikuwa njema kwa Yanga tangu dakika za mwanzo kutokana na makosa mengi yaliyokuwa yakifanywa na wachezaji wake pengine kutokana na kukumbwa na presha ya mchezo.

Yanga iliruhusu bao la kwanza kwenye dakika ya 11 baada ya shuti la nje ya 18 lililopigwa na Lenponye Tshilerets kumshinda mlinda lango Ramadhani Kabwili na kutinga kimiani.

Yanga ilirejea mchezoni kwenye dakika ya 30 kwa Obrey Chirwa kuisawazishia akipokea pasi murua kutoka kwa Papi Tshishimbi.

Kipindi cha pili ni Township Rollers iliyofanikiwa zaidi kwani licha ya kutawala mchezo huo, ilikuwa hatari katika mashambulizi ya kushitukiza kupitia kwa washambuliaji wake wa pembeni.

Alikuwa Sikele aliyeifungia Rollers bao la pili kwenye dakika ya 82 baada ya Rollers kupiga mpira wa pasi nyingi kabla mfungaji hajapewa pasi mpenyezo na kuukwamisha mpira wavuni kiurahisi kabisa

Matokeo hayo yanailazimu Yanga ikapate ushindi ugenini wa kuanzia mabao 2-0 ili iweze kufuzu hatua ya mtoano.

Timu hizo zitarudiana baada ya siku 10, March 17 huko nchini Botswana.

Timu itakayotolewa kwenye hatua hiyo itatupwa katika michuano ya kombe la Shirikisho na mshindi atatinga hatua ya makundi.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
6h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
10h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
15h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
15h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’