Bado Kamusoko tu

Yanga Damu By Yanga Damu
•
19 Jul 2017
Bado Kamusoko tu
Yanga imeanza kujifua wiki iliyopita ikiwa ni maandalizi ya msimu mpya wa VPL pamoja na mchezo wa Ngao ya Jamii Agosti 23 dhidi ya Simba.

Jumla ya wachezaji 16 wako kikosini wakiendelea na mazoezi.

Lakini bado kiungo fundi Thabani Kamusoko hajarejea kutoka Zimbwabwe. Mkataba wa kiungo huyo umemalizika na tayari uongozi umeshamalizana nae juu ya kusaini mkataba mpya.

Imeelezwa wakati wowote atatua jijini Dar es salaam kusaini mkataba mpya.

Wachezaji ambao wako kambini wakiendelea na mazoezi ni wapya wanne; kipa Mcameroon, Youthe Rostand aliyesajiliwa kutoka African Lyon, beki Abdallah Hajji ‘Ninja’ kutoka Taifa Jang’ombe, kiungo Pius Buswita kutoka Mbao FC na mshambuliaji Ibrahim Ajib kutoka kwa mahasimu, Simba SC.

Wengine ni mabeki, Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Juma Abdul, Pato Ngonyani, Mwinyi Hajji Mngwali, Andrew Vincent ‘Dante’.

Viungo Geoffrey Mwashiuya, Juma Mahadhi, Said Juma Makapu, Emmanuel Martin, Yussuf Mhilu, Obrey Chirwa na mshambuliaji Amissi Tambwe.

Pia wamo Henry Okoh kutoka Nigeria na Fernando Bongnyang kutoka Cameroon ambao wanafanya majaribio.

Wachezaji ambao hawapo ni pamoja na majeruhi wawili, kipa Benno Kakolanya na kiungo Deus Kaseke; mshambuliaji Donald Ngoma amesharejea na ataanza mazoezi wakati wowote.

Beki Hassan Kessy na winga Simon Msuva wapo na kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars ambacho leo Jumatano kinakwenda Kigali, Rwanda kwa ajili ya mchezo wa marudiano na Rwanda mwishoni mwa wiki kuwania tiketi ya CHAN 2018 nchini Kenya.

Aidha Winga Simon Msuva hatakuwepo kwenye kikosi cha Yanga msimu ujao baada ya kusajiliwa na klabu ya Difaa El Jadida ya Morocco.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
6h ago
READ MORE →
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE →
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE →
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
14h ago
READ MORE →
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
17h ago
READ MORE →
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
18h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
21h ago
READ MORE →
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE →
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE →
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE →