Katika mchezo wa Ngao ya Jamii mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele alikaribia kuwa mchezaji wa pili kufunga hat-trik katika mchezo wa watani wa jadi pale alipofunga mabao mawili katika ushindi wa mabao 2-1
Mayele anawania rekodi hiyo iliyowahi kuwekwa na Mzee Abdallah Kibaden miaka ya 70 wakati akiitumikia Simba
Akiwa katika msimu wake wa pili na Yanga, Mayele ni miongoni mwa wachezaji wenye idadi kubwa ya mabao katika mechi za watani wa jadi
Ana mabao matatu kibindoni yote akiyafunga katika mechi za Ngao ya Jamii
Jumapili Mayele atakuwa akiwania kuwafunga Simba kwenye ligi lakini pia kama alikaribia kupiga hat-trik kwenye Ngao ya Jamii, hii ni nafasi nyingine kwake
ADVERTISE HERE