Wananchi wamezisikia kauli zisizo za kiuanamichezo zinazotolewana Msemaji wa Simba Ahmed Ally kuelekea mchezo wa watani wa jadi utakaopigwa kesho Jumapili katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Jambo jema ni kuwa Ali Kamwe na kitengo cha habari na mawasiliano, wameamua kukaa kimya kumuacha amalize maneno yote! Lakini pasipo na shaka majibu yake atayapata pale uwanja wa Benjamin Mkapa siku ya Jumapili
Imekuwa ni kawaida kwao kuwa na maneno mengi kabla ya mchezo lakini baada ya dakika 90 wengine hukwepa kabisa hata kuzungumza na vyombo vya habari
Huu ni utaratibu ambao Haji Manara aliuweka wakati akiwa msemaji wa Simba, hata hivyo yeye mwenyewe baada ya kujiunga na Yanga aliuacha kwa sababu anafahamu mechi ya mpira wa miguu haichezwi kwenye vyombo vya habari
Kambi ya Yanga imekuwa na utulivu mkubwa kwenye maandalizi yao kuelekea mchezo dhidi ya Simba
Yanga inakwenda kuikabili Simba ikiwa na malengo, USHINDI ili kunogesha sherehe za ubingwa!