Ushindi ndio matokeo ya muhimu zaidi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Mar 2018
Ushindi ndio matokeo ya muhimu zaidi
Muda mfupi ujao, kikosi cha Yanga, mabingwa wa Tanzania Bara kinashuka kwenye uwanja wa Taifa kuwakabili mabingwa wa Botswana Township Rollers kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa raundi ya kwanza.

Yanga inahitaji zaidi matokeo ya ushindi katika mchezo huu unaopigwa kwenye dimba lake la nyumbani.

Ili kuhakikisha hilo linafanikiwa, kocha Mkuu wa Yanga George Lwandamina ameanza na kikosi ambacho kwa kiasi kikubwa kimeisaidia Yanga kutofungwa katika michezo tisa iliyopita kwenye michuano yote ikiwa ni pamoja na kushinda michezo sita mfululizo katika ligi kuu ya Vodacom.

Aidha amefanya mabadiliko kwenye nafasi ya mlinda lango ambapo amemuanzisha kinda Ramadhani Kabwili akimpumzisha mlinda lango namba moja, Youthe Rostand.

Huu ni mchezo wa pili kwa Kabwili kudaka kwenye michuano hiyo baada ya pia kukaa langoni kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya St Louis uliopigwa katika dimba hilo hilo la taifa.

Kiraka Said Juma 'Makapu' ameendelea kucheza nafasi ya beki wa kati kufuatia kukosekana kwa Andrew Vicent ambaye ni majeruhi.

Pato Ngonyani atashirikiana na Papi Tshishimbi katika kiungo wakisaidiwa na viungo washambuliaji Ibrahim Ajib, Pius Buswita na Emanuel Martin.

Obrey Chirwa amerejea kikosini baada ya kukosa michezo mitatu kutokana na majeruhi.

Yanga ina matumaini makubwa ya kuibuka na ushindi katika mchezo huo ambao baada ya dakika 90 kumalizika huenda mwanga wa kutinga hatua ya makundi ukaanza kuangaza.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’