Baada ya ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Kagera Sugar, kikosi cha Yanga hakina muda wa kupoteza kwani jana waliingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo unoafuata Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Simba. Mchezo huo utapigwa Jumapili, April 16 2023 saa 11 jioni
Mechi muhimu kwa Yanga kushinda ili kujihakikishia ubingwa wa 29 wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara
Wananchi wako kileleni mwa msimamo wa ligi wakiwa na alama 68 alama nane zaidi ya Simba inayoshika nafasi ya pili ikiwa na alama 60
Baada ya mchezo dhidi ya Simba, zitabaki mechi nne kuhitimisha msimu na iwapo Yanga itashinda siku ya Jumapili, itahitaji alama mbili tu kutoka mechi nne zilizobaki
Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze amesema wanatambua ushindi utawaweka katika nafasi nzuri ya kutetea ubingwa
Ni muhimu kwao kuwa katika mazingira hayo kabla ya kuelekea Nigeria kuikabili Rivers United kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza robo fainali michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika
Yanga inashikilia rekodi ya aina yake kwenye derby ikiwa haijapoteza mchezo wowote wa ligi kuu dhidi ya Simba tangu mwaka 2019



